Matumizi ya Ushairi katika Tamthilia ya Kiswahili

Wanyela, S. James (2008) Matumizi ya Ushairi katika Tamthilia ya Kiswahili. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Matumizi ya Ushairi katika Tamthilia ya Kiswahili)
2016-02-140.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (80MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu umechunguza matumizi ya ushairi katika tamthilia ya Kiswahili. Uchunguzi umejiegerneza katika tamthilia tatu 1.;1 Kiswahili: Mama ee (1987), Kilio cha Haki (1981) na Amezidi (1995). Malengo ya tasnifu hii yalikuwa kuchunguza umuhimu wa ushairi katika kuendeleza utanzu wa tamthilia ya Kiswahili. Aidha kudhihirisha jinsi ushairi ulivyotumiwa kusawiri ujumbe, lugha na wahusika katika tamthilia ya Kiswahili. Hatimaye kuonyesha kwamba -;ushairi ni mojawapo ya mbinu zinazotumiwa na watunzi wa tamthilia kama mbinu ya kimtindo. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile ya utanzu (Genre theory) ambayo inaeleweka kama kiainishi cha kundi aina, namna au mtindo wa utendaji wenye kuwasiliana. Kuainishwa na kujulikana kuwa mali ya kundi husika hutokana na sifa bainifu za umbo lake na kuendelezwa kwake. Warasmi kama Aristotle wanasema kwamba tanzu za fasihi zilikuwa tatu tu yaani shairi la hisia, drama na tendi. Tanzu hizi zilikuwa na ukuruba mkubwa mno.Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi imeshughulikia swala la utafitisababu za kuichagua mada, upeo wa utafiti, madhumuni ya utafiti,msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti.Sura ya pili imejadili matumizi ya ushairi katika usawiri wa ujumbe namatumizi ya lugha ya Kishairi katika tamthilia hizo tatu. Sura ya nne,mtafiti amejadili umuhimu wa ushairi katika kusawiri wahusika katika tamthilia. Utafiti ulifanywa kwa kutazama jinsi ushairi ulivyotumiwa na wahusika hao kuendeleza madhumuni ya mchezo. Sura ya tano ni hitimisho. Mtafiti ametoa muhtasari. matokeo kuhusu utafiti na mapendekezo ya utafiti zaidi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > P Philology. Linguistics
P Language and Literature > PE English
P Language and Literature > PJ Semitic
Depositing User: Geoffrey Obatsa
Date Deposited: 07 Apr 2017 11:18
Last Modified: 07 Apr 2017 11:18
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/1445

Actions (login required)

View Item View Item