Mnyambuliko Wa Vitenzi Vya Kigiryama Mtazamo Wa Fonolojia Leksishi

Ngowa, Nancy Jumwa (2008) Mnyambuliko Wa Vitenzi Vya Kigiryama Mtazamo Wa Fonolojia Leksishi. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Mnyambuliko wa Vitenzi vya Kigiryama: Mtazamo wa Fonolojia Leksishi)
Mnyambuliko Wa Vitenzi Vya Kigiryama Mtazamo Wa Fonolojia Leksishi.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (40MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu umechanganua mnyambuliko wa vitenzi vya Kigiryama kwa madhumuni ya kumulika taratabu zinazohusika. Uchanganuzi wa maelezo yametegemea mtazamo wa Fonolojia Leksishi katika nadharia ya Fonolojia inayozingatia falsafa ya kijumla ya Sarufi Zalishi. Deta ya kimsingi ya utafiti huu ni ya nyanjani. Deta hii imekusanywa kwa kutumia mbinu ya uhusisha na usikilizaji, ambapo mtafiti ametumia mazungurnzo ya kawaida. Uwasilishi wa data umezingatia maelezo ambayo yamesaidiwa na majedwali na michoro matawi. Tasnifu hii imepangwa katika sura nne. Sura ya kwanza inashughulikia utangulizi wa utafiti kwa kuzingatia misingi ya utafiti wenyewe ikiwemo swala la utafiti, malengo ya utafiti, tahadharia, upeo na mipaka ya utafiti, misingi ya nadharia na mbinu za utafiti. Katika srua ya pili, vigezo vya fonolojia ya Kigiryama vimezingatiwa Sura ya tatu imejikita katika uchanganuzi wa taratibu na vigezo vya vitenzi vya Kigiryama. Hatimaye, sura ya nne imetamatisha utafiti kwa kuonyesha matokeo ya utafiti ambayo yamedhihirisha kwamba, mnyambuliko wa vitenzi umeongozwa na kanuni bayana za Fonolojia Leksishi. Mchango wa kimsingi wa uchanganuzi huu umeegemea nadharia ya Isimu ya Fonolojia Leksishi kwa kudhihirisha umwafaka wake katika kuchanganua mnyambuliko wa vitenzi. Ujuzi huu ni muhimu katika uwanja wa isimu kwajinsi ambavyo unaweza kutumia katika isimu tumikizi katika uundaji wa kamusi.zaidi ya hayo, utafiti huu unaweza kutumika katika isimu linganishi na katika miradi ya kutafsiri lugha.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > P Philology. Linguistics
P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 14 Dec 2017 07:23
Last Modified: 14 Dec 2017 07:23
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/2909

Actions (login required)

View Item View Item