Ufasiliwa Msamiati Wa Kiimenti Kwa Wapokezi Wagichuka: Tathmini Katika Muuga FM

Muchiri, Muchuru Rukenya (2014) Ufasiliwa Msamiati Wa Kiimenti Kwa Wapokezi Wagichuka: Tathmini Katika Muuga FM. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Ufasiliwa Msamiati Wa Kiimenti Kwa Wapokezi Wagichuka: Tathmini Katika Muuga FM.)
2016-02-116.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (86MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu umechanganua msamiati msingi wa lahaja moja ya Kimeru iitwayo Kiimenti ili kutathmini vile unavyowaarifu wasikilizaji wa lahaja nyingine ya Kimeru iitwayo Gichuka, Swala kuu la utafiti limekuwa kubainisha kama wasikilizaji wa Muuga FM wa lahajaya Giehuka wanaarifiwa na taarifa za habari zinaposomwa kwa lahaja ya Kiimenti. Malengo ya utafiti yamekuwa kuubainisha msamiati msingi wa lahaja ya Kiimenti unaotumiwa katika habari za redio ya Muuga FM, kuonyesha mahusiano yake ya kisemantikina kudhihirisha vile unavyofasiliwa na wasikilizaji wa lahaja ya Gichuka,IIi kufikia malengo haya, data ya habari ilikusanywa kutoka redio ya Muuga FM. Data imechanganuliwa kupitia kiunzi eha nadharia, Nadharia za Isimu Amilifu Mfumo na Mahusiano Fahiwa zimetumiwa kuehanganua umbo la kiisimu la msamiati msingi wa Kiimenti nayo Tahakiki Usemi ikatumiwa kutathmini tendo la uarifu. Utafiti umefanyiwa maktabani na nyanjani. Walengwa walikuwa wasikilizaji wa redio ya Muuga FM wa lahaja ya Gichuka, Wahojiwa walitoka mji wa Chuka. Vigezo vya umri, jinsia na elimu vilitumiwakuwateua Sura ya kwanza imejumuisha usuli wa mada na taratibu zilizofuatwa ili kufanikisha utafiti, sura ya pili imeshughulikia muundo wa msamiati wa Kiimenti, sura ya tatu ikachanganua maana na mahusiano ya msamiati msingi wa Kiimenti. Nayo sura ya nne ikaonyesha vile unavyofasiliwa na wasikilizaji wa habari wa lahaja ya Giehuka. Sura ya tano imeshughulikia mahitimisho ya utafiti na kutoa mapendekezo. Matokeo ya utafiti yameonyesha kwamba wasikilizaji wengi wa lahaja ya Giehuka hutatizika wanapojaribu kufasili habari zinaposomwa kwa lahaja ya Kiimenti. Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kwa majedwali, miehoro na maelezo. Inatarajiwa kwamba utafiti huu utawafaa wasomi wa lugha na watafiti wa lahaja mbalimbali. Aidha, utawafaa watayarishi wa vipindi vya rediovinavyohusu lugha za kiasili.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > P Philology. Linguistics
Divisions: Africana
Depositing User: Geoffrey Obatsa
Date Deposited: 03 Feb 2017 10:40
Last Modified: 03 Feb 2017 10:40
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/1412

Actions (login required)

View Item View Item