Uhalisi na Mtindo Waken Walibora Katika Fasihi ya Watoto

Kairu, Winnifred Mukami (2005) Uhalisi na Mtindo Waken Walibora Katika Fasihi ya Watoto. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Uhalisi na Mtindo Waken Walibora Katika Fasihi ya Watoto)
2016-02-144.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (79MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu umeshughulikia uhalisi na mtindo wa Ken Walibora katika vitabu vya Ndoto ya Amerika (2001), Mgomba Changaraweni (2003), na Mtu wa Mvua (2003). Utafiti huu uliongozwa na nadharia mseto ya mtindo, maadili na uhalisia. Nadharia hizi zilifaa katika utafiti huu, huku ikichukuliwa ya kwamba kazi za watoto zinahitaji kuangaliwa katika mikabala mbalimbali.Tasnifu hii ina jumla ya sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo mada ya utafiti, malengo ya utafiti, tahadhania, sababu za kuchagua mada na misingi ya nadharia zimefafanuliwa. Aidha, yaliyoandikwa kuhusu mada hii na fasihi ya'. watoto yamejadiliwa ili kushadidia pengo la utafiti huu. Upeo na rnipaka ya utafiti .imefafanuliwa. RaE kadhalika, mbinu za utafiti ukiwemo utafiti wa maktabani pamoja na uchanganuzi wa data muhimu zimefafanuliwa. Sura ya pili imejadili fasihi ya watoto na maendeleo yake nchini Kenya. Vilevile, uhakiki katika fasihi ya watoto na sifa zake bainifu zimefafanuliwa. Aidha, majukumu ya mhakiki wa fasihi ya watoto pia yamefafanuliwa. Sura ya tatu ya utafiti huu imejadili, dhamira, maudhui na mafunzo ya kimaadili katika hadithi fupi za mwandishi Walibora.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > PZ Childrens literature
Divisions: Africana
Depositing User: Geoffrey Obatsa
Date Deposited: 25 Apr 2017 14:19
Last Modified: 25 Apr 2017 14:19
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/1449

Actions (login required)

View Item View Item