Mchango wa Mbazi za Biblia katika Ukuzaji wa Fasihi Andishi ya Kiswahili

Kiprotich, Priscah Jebet (2013) Mchango wa Mbazi za Biblia katika Ukuzaji wa Fasihi Andishi ya Kiswahili. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Mchango wa Mbazi za Biblia katika Ukuzaji wa Fasihi Andishi ya Kiswahili)
2016-02-147.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (79MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu unabainisha baadhi ya mbazi za Biblia na kuchanganua jinsi mbazi hizi zilivyotumiwa katika baadhi ya kazi za fasihi andishi ya Kiswahili. Katika kufanya hivyo, mchango wa mbazi za Biblia juu ya maandishi na matendo katika baadhi ya kazi za fasihi ya Kiswahili ulionyeshwa. Utafiti huu unaonyesha jinsi mbazi za Biblia zinavyochangia katika ukuzaji wa maudhui na mtindo katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mbazi ni hadithi fupi yenye masimulizi yanayolenga kutoa funzo au maadili fulani kwa wahusika. Mbazi nyingi hupatikana katika Biblia na zilitumiwa na Yesu Kristo katika mafunzo yake. Mbazi zina sifa bainifu za tanzu za fasihi na hivyo zinahitaji kueleweka katika muktadha na matini za fasihi ya Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya naratolojia na nadharia ya ufasiri ya hemenitiki. Nadharia ya naratolojia katika simulizi na usimulizi inadai kwamba ni sharti kuwa na kile kitendo cha kusimulia katika hadithi na lazima kuwe na mpangilio au mfuatano wa matukio katika simulizi yenyewe. Naratolojia katika mbazi inahusu usimulizi wa mbazi zenyewe na jinsi mtindo huu unavyodhihirika katika kazi za fasihi zilizochambuliwa. Nadharia ya hemenitiki inahusiana na ufasiri wa maana. Nadharia hii ilisaidia kuchanganua ufasiri wa maana katika matini zilizoteuliwa. Mtafiti alifanya utafiti maktabani kwa kusoma maandishi yaliyohusiana na mada hii na kuchuja data na habari muhimu. Matokeo ya utafiti huu yamewasilishwa kwa maelezo ya kinathari. Tasnifu hii ina sura saba ambazo zimejengeka kutokana na sura ya kwanza. Sura hizi zinaonyesha umuhimu wa mbazi katika kazi za fasihi ya Kiswahili kwa kuzingatia vipengele vya maudhui na mtindo. Tunatarajia kwamba matokeo ya utafiti huu yatakuwa ya manufaa kwa wapenzi wa fasihi katikajamii ya sasa.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > PI Oriental languages and literatures
P Language and Literature > PN Literature (General)
Divisions: Africana
Depositing User: Geoffrey Obatsa
Date Deposited: 28 Apr 2017 12:22
Last Modified: 28 Apr 2017 12:22
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/1452

Actions (login required)

View Item View Item