Ukiushi katika Ushairi wa Amri Abedi Na Kithaka Wa Mberia

Njuguna, Helina Wanjiku (2015) Ukiushi katika Ushairi wa Amri Abedi Na Kithaka Wa Mberia. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Ukiushi katika Ushairi wa Amri Abedi Na Kithaka Wa Mberia)
2016-02-149.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (79MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu umeshughulikia matumizi ya ukiushi katika mashairi teule ya Kithaka wa Mberia na Amri Abedi. Utafiti unazingatia diwani mbili za Mashairi: Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri (1954) na Mchezo wa Karata (1997). Uteuzi wa diwani hizo ulifanywa kwa kutumia mbinu kusudio kwa kuwa zilidhihirisha matumizi ya ukiushi ambayo yangetosheleza mahitaji ya utafiti. Utafiti ulizingatia matumizi ya ukiushi wa msamiati, sarufi, maumbo na awamu ya kihistoria katika mashairi husika. Utafiti uliongozwa na nadharia changamano: Nadharia ya Kimtindo na Nadharia ya Kihemenitiki. Mihimili ya Nadharia ya Kimtindo kama alivyoeleza Leech (1969) ilitumika katika kubainisha aina za ukiushi zilizotumika katika utunzi wa mashairi husika. Mihimili ya Nadharia ya Kihemenitiki ilimwongoza mtafiti katika ufasiri wa ujumbe wa mashairi. Maana ya shairi ilipatikana kwa kuzingatia muktadha wake wa kilugha na kuuhusisha na shairi zima. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo ambapo uchanganuzi ulizingatia matumizi ya ukiushi wa msami ati katika mashairi huru na ya arudhi. Aidha, uchanganuzi ulishughulikia ukiushi wa sarufi na maumbo katika mashairi huru. Vilevile, ulizingatia ukiushi wa awamu ya kihistoria katika mashairi ya arudhi. Utafiti uligundua kuwa ukiushi wa msami ati umetumiwa katika mashairi ya Abedi na Mberia lakini uteuzi wao wa msamiati ni tofauti. Rata hivyo, umetumiwa kuchimuza ujumbe wao. Ukiushi wa sarufi umebainika katika mashairi huru teule. Ukiushi huu umetumiwa kusisitiza ujumbe pamoja na kuyapa mashairi mahadhi. Ukiushi wa maumbo umedhihirika katika mashairi huru kupitia sitiari za kimchoro. Ukiushi huu umetumiwa kuchimuza na kusisitiza ujumbe. Ukiushi wa awamu ya kihistoria umepatikana katika mashairi ya arudhi kupitia matumizi ya maneno ya kilahaja na yale yenye asili ya Kiarabu. Matumizi ya ukiushi huu yanafanikisha urari wa vina na mizani. Utafiti umetoa mchango katika maswala ya lugha ya mashairi hasa kwa kulinganisha matumizi ya ukiushi katika mashairi huru na ya arudhi Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidi ufanywe katika kazi za watunzi wengine wa mashairi. Pia, utafiti ufanywe kwa kuzingatia aina zingine za ukiushi kama vile wa sauti, sajili na maana katika kazi husika.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
P Language and Literature > PN Literature (General)
Divisions: Africana
Depositing User: Geoffrey Obatsa
Date Deposited: 28 Apr 2017 12:30
Last Modified: 28 Apr 2017 12:30
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/1454

Actions (login required)

View Item View Item