Omutimba, Charles Washiali (2015) Usimulizi Katika Riwaya za; Adili na Nduguze, Walenisi na Babu Alipofufuka. Masters thesis, Kenyatta University.
PDF (Usimulizi Katika Riwaya za; Adili na Nduguze, Walenisi na Babu Alipofufuka)
2016-02-157.pdf - Accepted Version Restricted to Repository staff only Download (78MB) | Request a copy |
Abstract
Usimulizi ni dhana iliyohusishwa kwa muda mrefu na hadithi. Hadithi ni mojawapo ya tanzu za fasihi simulizi, ambayo hutolewa kwa maelezo ya nathari. Huhusisha vipera kama vile; ngano, rnighani, hurafa, hekaya, visasili, visakale ngano za mtanziko na visa vingine. Kihistoria, fasihi ya Kiafrika ilisimuliwa na kupitishwa kwa vizazi kwa njia ya mdomo na kuhifadhiwa katika kurnbukumbu. Fasihi andishi ni utanzu mpya uliokuja kufuatia kuanzishwa kwa maandishi ili kuweza kuhifadhi sanaa ya fasihi ya Kiswahili. Riwaya kwa hivyo, ni ngeni katika Kiswahili kwa vile ililetwa na majilio ya hati za kirurni zilizoletwa na Wazungu na kuturnika kuihifadhi fasihi. Utafiti mwingi uliofanywa unaonyesha kuwa, riwaya ambayo huturnia maelezo ya nathari inaelekea kuwiana na simulizi na wengine wanapinga kabisa kuwa, hakuna uhusiano kati ya riwaya na simulizi. Hata hivyo, kumezuka riwaya mbalimbali katika nyakati mbalimbali ambazo zimetatiza ufasiri na uhakiki wake. Kwa sababu ya riwaya kuwa ya nathari kama ngano, yawezekana sifa za usimulizi zipatikanazo katika simulizi (zilizo pia na mtindo wa nathari) kuturnika katika utunzi na uhakiki wa riwaya ya Kiswahili. Ifaharnikavyo ni kuwa, simulizi zina muundo maalumu wa kifomyula ambao zinaturnia kupitisha ujumbe wake na hivyo, kuna makisio kuwa, ndani yake kuna vipengele maalumu vinavyoweza kuturniwa kufasiri vipengele muhimu riwayani. Hadithi ndizo zinazohusishwa sana na rniundo na maumbo ya usimulizi. Katika uhakiki wa ngano uliosharniri huko Ulaya, walihakiki masimulizi kifomyula. Hata hivyo, uhakiki wa riwaya umefungika kwa muda mrefu kwa rnisingi ya maudhui, wahusika na mtindo huku umbo na muundo wake ukipuuzwa, hali ambayo inaathiri ufasiri na uhakiki wake. Kuna haja ya kutalii nafasi ya rniundo na maumbo ya usimulizi katika riwaya ili kuyahusisha na utunzi na uhakiki wake na kupata uelewa wa kina kuihusu.
Item Type: | Thesis (Masters) |
---|---|
Subjects: | P Language and Literature > PN Literature (General) |
Divisions: | Africana |
Depositing User: | Geoffrey Obatsa |
Date Deposited: | 28 Apr 2017 12:53 |
Last Modified: | 28 Apr 2017 12:53 |
URI: | http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/1463 |
Actions (login required)
View Item |