Athari ya Duksi katika Ukufunzi wa Ujifinzaji wa Kiswahili: Mtazamo wa Uchanganuzi Linganishi

Wenyaa, Nesaba Salome (2007) Athari ya Duksi katika Ukufunzi wa Ujifinzaji wa Kiswahili: Mtazamo wa Uchanganuzi Linganishi. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Athari ya Duksi katika Ukufunzi wa Ujifinzaji wa Kiswahili: Mtazamo wa Uchanganuzi Linganishi)
Athari ya duksi katlka ufunzaji na ujifunzaji wa kiswahili mtazamo wa uchanganuzi linganishi.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (78MB) | Request a copy

Abstract

Kazi hii imekusudia kuchanganua athari ya elimu ya Duksi katika ufunzaji na ujifunzaji wa sarufi ya lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa mtazamo wa nadharia ya Uchanganuzi Linganishi. Vipengele vya kisarufi yaani abjadi, maendelezo, msamiati, mtindo wa kuandika, mpangilio wa maneno katika sentensi ndivyo vilivyochunguzwa katika utafiti huu. Sampuli mseto ndiyo iliyochaguliwa na kuhusishwa. Watafiti walioshirikishwa walitoka katika wilaya ya Garissa, mjini pamoja na viunga vyake. Tajriba, imani, elimu, mielekeo na maoni ya wanajamii wa viwango mbalimbali yalizingatiwa. Kazi hii pia ilizingatia mbinu za kufunzia Kiswahili madhumuni yakiwa ni kuboresha na kuimarisha ufunzaji na ujifunzaji wa lugha hii katika mkabala wa mazingira ambapo lugha ya Kiarabu inazingatiwa. Yaani hutumiwa kwa kuendeshea shughuli za kidini. Kutokana na utafiti huu ilibainika kuwa elimu ya Duksi ina athari chanya na hasi. 'Mbinu za kufunzia zimedhihirisha njia tofauti tofauti zinazoweza kusaidia kuinua kiwango cha kufunza lugha. Papo hapo kutokana na ukinzano kati ya vipengele vya kisarufi vya (Kiarabu na Kiswahili), imetambulikana kuwa wanafunzi hupata shida zinazohusiana na abjadi, maendelezo, hijai, msamiati na maana ya sentensi. Utafiti huu umependekeza kuwa bado Kuna haja ya kuendeleza elimu jumuifu . ambapo mbinu changamano zinaweza kutumika. Hii ni kwa sababu mafunzo hayo yote ya kidini na ya kimagharibi yana manufaa kwa maisha ya wanafunzi wakiwa shuleni na hata baada ya masomo shuleni.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > P Philology. Linguistics
P Language and Literature > PI Oriental languages and literatures
Divisions: Africana
Depositing User: Geoffrey Obatsa
Date Deposited: 13 Sep 2017 06:25
Last Modified: 13 Sep 2017 06:25
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/2080

Actions (login required)

View Item View Item