Mogeni, Magoma Erick (2015) Fani na Maudhui katika Mashairi ya Magazeti ya Taifa Leo. Masters thesis, Kenyatta University.
![]() |
PDF (Fani na Maudhui katika Mashairi ya Magazeti ya Taifa Leo)
Fani na maudhui katika mashairi....pdf - Accepted Version Restricted to Repository staff only Download (62MB) | Request a copy |
Abstract
Utafiti huu umeshugulikia tani na maudnui katika mashairi ya magazeti ya Taifa LeoJumamosi na Taifa Jumaplii katika kipindi cha mwaka 2010-2012. Katika fasihi ya Kiswahili kila mwandishi ana njia yake ya kipekee ya kuwasilisha kazi yake. Kuna wale wanaoeleza yaliyotendeka katika jamii kwa uaminifu na kwa namna ambayo atakayesorna kazi yake ataona ni mambo ya kuaminika au yaliyo na uwezo wa kutendeka katika jamii. Pia, kuna wasanii wengine ambao huelezea matukio halisi lakini kwa njia ya kiubunifu. Ingawa hivyo wasanii hawa wote hulenga kupitisha uiumbe kwa hadhira yao. Magazeti ya Taifa Leo huendeleza maudhui mengi kupitia mashairi yake; kwa mfano siasa, uchumi, utamaduni, mazingira, elimu, dini na mengine mengi. Hivyo utafiti huu umechunguza fani na maudhui yaliyoshughulikiwa na Magazeti ya Taifa Leo mwaka 2010-2012. Ulilenga kubainisha maudhui ya Magazeti ya Taifa Leo usawiri wao na hatimaye kuonyesha nafasi ya Magazeti ya Taifa Leo katika maendeleo ya mashairi nchini Kenya. Nadharia iliyotumiwa ni lie ya kimtindo ya kirasimi inyoasisiwa na Leech na Short (1981). Nadharia hii imeteuliwa kwa msingi kuwa mihimili yake ilituwezesha kuchunguza maudhui tulivoteua katika mashairi ya Magazeti ya Taifa Leo ili kuafiki malengo yetu. Data iliyotumiwa katika utafiti huu ilikusanywa maktabani ambapo mapitio ya vitabu, majarida, magazeti na tasnifu yalisaidia katika kuupa msingi utafiti huu. Magazeti teule ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili yaliteuliwa kwa msingi kuwa yalikuwa na mashairi yenve maudhui ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulifanywa kupitia maelezo.
Item Type: | Thesis (Masters) |
---|---|
Subjects: | P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania |
Divisions: | Africana |
Depositing User: | Tim Khabala |
Date Deposited: | 18 Sep 2017 14:14 |
Last Modified: | 18 Sep 2017 14:14 |
URI: | http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/2276 |
Actions (login required)
![]() |
View Item |