Maudhui na Mitindo ya Lugha Inayotumiwa Kuwasilisha Mafunzo ya Kukuza Vijana Katika Misingi ya Kiuana: Dhehebu la P.C.E.A–Kikuyu

Kibutu, Salome Wambui (2013) Maudhui na Mitindo ya Lugha Inayotumiwa Kuwasilisha Mafunzo ya Kukuza Vijana Katika Misingi ya Kiuana: Dhehebu la P.C.E.A–Kikuyu. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Maudhui na Mitindo ya Lugha Inayotumiwa Kuwasilisha Mafunzo ya Kukuza Vijana Katika Misingi ya Kiuana: Dhehebu la P.C.E.A–Kikuyu)
2016-02-108.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (87MB) | Request a copy

Abstract

Asasi za kidini zimechangia pakubwa katika kuwapa vijana mafunzo kuhusu maisha yao. Mojawapo ya asasi hizo ni dhehebu la P.C.E.A - Kikuyu. Kupitia kwa mafunzo hayo, kanisa hilo limeendeleza vijana kiuana. Utafiti huu umechunguza maudhui na mitindo ya lugha iliyotumika katika kuwasilisha mafunzo hayo. Data ilikusanywa na kuchanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Semeotiki. Kadhalika, mbinu shirikishi nyanjani ilitumika katika kupata data. Mbinu zilizohitajika kutumika kuwasilisha maudhui zilihusisha matumizi ya lugha ishara kama vile vielelezo. Tamathali mahususi za usemi kama vile tashibihi, sitiari na jazanda zilitumika ili kujenga muktadha wa kuwasaidia vijana kuelewa ujumbe uliokusudiwa. Aidha, lugha mwiko, lugha ya utani na ucheshi, lugha dadisi na lugha ya marejeleo zilitumika na ilisaidia kufanikisha mawasiliano. Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kuwa maudhui ambayo hujitokeza katika mafunzo kwa vijana ni muhimu kwa vile huwasaidia katika kukabiliana na matatizo ambayo yameshuhudiwa katika jamii ya kisasa. Baadhi ya maudhui hayo ni utumiaji wa dawa za kulevya, ponografia na mauaji ya kifantasia, Ukimwi, mila pamoja na utamaduni wa jamii. Pia, masuala ya uana, mahusiano baina ya vijana wa kike na kiume, vipawa, uaminifu katika jamii na uzalendo yalijadiliwa. Aidha, baadhi ya majukumu ya kiuana yalielezwa waziwazi. Jukumu la vijana kuwa wazazi lilifafanuliwa huku tofauti za kijinsia zikifafanuliwa. Umuhimu wa kuzingatia nidhamu, heshima na haki kwa wote bila kujali jinsia au ukabila ni baadhi ya mambo ambayo yalitiliwa mkazo. Uajibikaji na umuhimu wa elimu kwa wote, kufanya kazi maishani bila kujali jinsia ni dhima zilizofunzwa vijana. Mafunzo wanayopewa vijana katika dhehebu la P.C.E.A- Kikuyu yanasaidia kuwaelekeza vijana katika jamii. Huu ni mchango muhimu katika jamii ambao unapasa kuendelezwa na madhehebu mengine yanayopatikana nchini Kenya.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > PI Oriental languages and literatures
P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Geoffrey Obatsa
Date Deposited: 06 Oct 2017 10:37
Last Modified: 06 Oct 2017 10:37
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/2460

Actions (login required)

View Item View Item