Matumizi ya Kiswahili katika Tarakilishi

Kamau, Stephen Njihia (2005) Matumizi ya Kiswahili katika Tarakilishi. Undergraduate thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Matumizi ya Kiswahili katika Tarakilishi)
Matumizi ya Kiswahili katika Tarakilishi.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (56MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu unashughulikia swala la matumizi ya Kiswahili katika tarakilishi; Katika kufanya hivyo, utafiti huu umechunguza kuhusu miradi mbali mbali ya matumizi ya Kiswahili katika tarakilishi katika maeneo ya Uropa, Marekani na Afrika Mashariki na Kati. Hatimaye, utafiti wenyewe umeonyesha njia mbali mbali ambazo kwazo teknolojia ya tarakilishi imekuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Nadharia ambazo zimeuongoza utafiti huu ni nadharia ya msambao wa uvumbuzi na ile ya utegemezi wa vyombo vya habari. Nadharia ya msambao wa uvumbuzi hujaribu kueleza jinsi teknolojia mpya mbali mbali husambaa katika jamii haswa kupitia lugha za jamii husika. Nayo nadharia ya utegemezi wa vyombo vya habari huonyesha jinsi jamii hutegemea kwa dhati vyombo vya habari katika kufanikisha mawasiliano katika jamii. Tasnifu hii ina jumla ya sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo tumeshughulikia mada ya utafiti, swala la utafiti, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, nadharia tete za utafiti na sababu za kuchagua mada. Aidha, tumejadili upeo na mipaka ya utafiti, msingi wa nadharia na yaliyoandikwa kuhusu mada hii. Mwisho, mbinu za utafiti zimefafanuliwa. Sura ya pili imeangazia juu ya baadhi ya miradi ya matumizi ya Kiswahili katika tarakilishi katika maeneo ya Uropa na Marekani. Mfano mzuri wa mradi uliopitiwa katika sura hii ni ule wa SALAMA ambao hutumika katika kuchanganua lugha ya Kiswahili kimofolojia, kupunguza utata katika matini za Kiswahili na pia kusahihisha makosa ya tahajia mbali na kufanya kazi za kutafsiri. Sura ya tatu imefafanua juu ya miradi ya matumizi ya Kiswahili katika tarakilishi katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Mradi wa kutajika hapa ni kama ule wa kampuni ya Microsoft East Africa wa kuunda msamiati wa Kiswahili kwa matumizi katika ~i. Miradi mingine ni kama vile mradi wa kugeuza matini za Kiswahili hadi usemi, uundaji wa injini pekuzi ya Kiswahili n.k. Katika sura ya nne utafiti huu umeweza kubainisha jinsi lugha ya Kiswahili ilivyokuzwa na kuendelezwa na teknolojia ya tarakilishi. Kiswahili kimekuzwa na kuendelezwa kwa njia kama vile uundaji wa istilahi mpya, uundaji wa kamusi za mtandao, ufundishaji wa Kiswahili katika mtandao n.k. Sura ya tano nayo inatoa muhtasari wa utafiti huu, changamoto za utafiti, mchango wa utafiti na mapendekezo kwa minajili ya utafiti wa baadaye. Kutokana na utafiti huu imebainika kuwa lugha ya Kiswahili kwa sasa ni miongoni mwa lugha chache ulimwenguni ambazo zinatumika katika mitambo ya tarakilishi. Pia, imebainika kuwa lugha ya Kiswahili imekuzwa na kuendelezwa na teknolojia ya tarakilishi ya njia mbali mbali. Mwisho kabisa kuna marejeleo ya utafiti na vile vile viambatisho vinafuata na kutufikisha kwenye mwisho wa utafiti.

Item Type: Thesis (Undergraduate)
Subjects: P Language and Literature > P Philology. Linguistics
P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
T Technology > T Technology (General)
Divisions: Africana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 08 Dec 2017 13:03
Last Modified: 08 Dec 2017 13:03
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/2848

Actions (login required)

View Item View Item