Mgongano wa Tamaduni katika Hadithi Fupi za Kiswahili

Wafula, Catherine Nanjala (2015) Mgongano wa Tamaduni katika Hadithi Fupi za Kiswahili. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Mgongano wa Tamaduni katika Hadithi Fupi za Kiswahili)
Mgongano wa Tamaduni katika Hadithi Fupi za Kiswahili.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (66MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu ulishughulikia swala la mgongano wa tamaduni katika hadithi fupi za Kiswahili. Mtafiti alihakiki kazi za waandishi teule wa hadithi fupi. Kazi zilizochanganuliwa ni kutokana na vitabu vinne vya hadithi fupi ambavyo ni pamoja na Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine kilichohaririwa na K.W.Wamitila(2004), Kiti cha Moyoni na Hadithi Nyingine kilichohaririwa na Ken Walibora na Said Mohamed(2007), Mwendawazimu na Hadithi Nyingine kilichohaririwa na Mwenda Mbatiah(2000) pamoja na Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine kilichohaririwa na Ken Walibora na Said Mohamed(2007). Utafti huu unaongozwa na nadharia ya udhanaishi. Udhanaishi ni falsafa inayoshughulikia masuala kuhusu maisha. Ni mtazamo unaokagua .kwa upembuzi hali na nafsi ya mtu katika ulimwengu anaoishi. Pia ni falsafa inayozungurnzia uhusiano uliopo kati ya mtu na Mungu na iwapo mtu anapaswa kuamini kuwepo kwa Mungu. Nadharia hii hujaribu kueleza uhuru wa mtu binafsi, uwezo wa mtu kujifikiria na kujiamulia ni wajibu wa binadamu katika ulimwengu. Kupitia nadharia hii ni dhahiri kwamba jinsia ya kike na kiurne wanaathiriwa pakubwa na utamaduni huu hasi. Rata hivyo kuna matumaini ikiwa binadamu mwenyewe atajinasua katika mtego huu kwa kuzielewa na kuzipigania haki zake.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: H Social Sciences > HM Sociology
P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 14 Dec 2017 07:14
Last Modified: 14 Dec 2017 07:14
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/2899

Actions (login required)

View Item View Item