Uarifu katika Taarifa za Habari: Mtazamo wa Isimu Amilifu

Sichangi, Geoffrey Mukhono (2008) Uarifu katika Taarifa za Habari: Mtazamo wa Isimu Amilifu. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Uarifu katika Taarifa za Habari: Mtazamo wa Isimu Amilifu)
Sichangi, Geoffrey Mukhono.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (74MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu umechambua matini ili kutathmini mafanikio ya uarifu katika taarifa za habari zinazosomwa kwa Kiswahili kwa madhumuni ya kuonyesha utoshelevu wa uarifu. Tumechanganua data kutoka kwenye vituo vya utangazaji vya KBC na Redio Citizen. Watafitiwa ambao walishirikishwa katika utafiti huu waliteuliwa kutoka eneo la Kahawa Sukari, wilayani Thika. Vigezo vya wasikilizaji wenye umri, elimu na jinsia tofauti vilitumika. Mchango wa kazi hii ulilenga kuziba penga katika isimu lililosababishwa na tatizo la ukosefu wa uarifu katika taarifa za habari zinazosomwa kwa Kiswahili. IIi kufanikisha utafiti huu, nadharia ya isimu amilifu ilitumika. Maana zinazotambuliwa na mtazamo wa Sarufi Amilishi Mfumo kwa mujibu wa Halliday zilitumika katika kuchanganua uarifu, huku vigezo vya umatini kwa mujibu wa Dressler na Beaugrande vikitumika katika kutathmini umatini wa taarifa za habari. Matokeo ya utafiti huu yamewasilishwa kwa njia ya maelezo, katika sura tatu. Imedhihirika katika utafiti huu ya kwamba taarifa za habari zinazawasilishwa katika Kiswahili huarifu kwa -kiasi kikubwa. Hata hivyo, uarifu katika taarifa za habari hutingwa zaidi na ukosefu wa kina katika habari, ukasefu wa ujumbe mpya pamoja na matumizi ya sentensi zisizofasirika kwa uwazi. Hatimaye, tumependekeza taratibu za kuboresha uwasilishaji wa taarifa hiza ili kufanikisha uarifu.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: H Social Sciences > HE Transportation and Communications
P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 13 Mar 2018 13:12
Last Modified: 13 Mar 2018 13:12
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/3516

Actions (login required)

View Item View Item