Ukoloni Mamboleo na Utanda Wazi katika Tamthilia Teule

Mwirabua, Andrew Kairi (2014) Ukoloni Mamboleo na Utanda Wazi katika Tamthilia Teule. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Ukoloni Mamboleo na Utanda Wazi katika Tamthilia Teule)
Mwirabua, Andrew Kairi.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (44MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu umechunguza jinsi ukoloni mamboleo unavyodhihirika katika muktadha wa utandawazi kwa kurejelea tamthilia mbili teule: Posa za Bikisiwa (2008) ya S. A. Mohamed na K. King'ei na Sudana (2006) ya Alamin Mazrui na K. Njogu. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Baada Ukoloni. Utafiti ulifanyiwa maktabani. Mtafiti alisoma makala mengi yaliyohusiana na mada ya utafiti ili kupata data iliyokusudiwa. Mtafiti pia alifanya utafiti wa nyanjani kwa kuwahoji watunzi. Vilevile, mtafiti aliwahoji wataalamu na wanafunzi wenzake. Aidha mtafiti alichanganua tamthilia hizi mbili teule ili kupata data iliyokusudiwa ili kutimiza matakwa ya utafiti huu. Data iliyokusanywa ilirekodiwa na kuchanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti na nadharia ya Baada Ukoloni. Data zilizokusanywa zimewasilishwa kwa njia ya maelezo. Kazi hii imewasilishwa kwa sura tano. Utafiti huu umeonyesha kwamba utandawazi ni mbinu mpya ya kisasa ya kuendeleza ukoloni mamboleo dhidi ya mataifa maskini.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 13 Mar 2018 13:02
Last Modified: 13 Mar 2018 13:02
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/3522

Actions (login required)

View Item View Item