Ulinganishaji wa Uwasilishaji wa Mashairi ya Euphrase Kezilahabi na Kithaka wa Mberia

Juma, Nyongesa Job (2015) Ulinganishaji wa Uwasilishaji wa Mashairi ya Euphrase Kezilahabi na Kithaka wa Mberia. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Ulinganishaji wa Uwasilishaji wa Mashairi ya Euphrase Kezilahabi na Kithaka wa Mberia)
Juma, Nyongesa Job.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (51MB) | Request a copy

Abstract

Tasnifu hii ililenga kufanya uchunguzi katika kazi mbalimbali za fasihi ya ushairi huru za Euphrase Kezilahabi na Kithaka Wa Mberia. Mitindo ilivyoangaliwa katika utafiti huu ni mitindo ya taswira, jazanda na takriri. Tathimini ikiwa kama mitindo hii ina ufanano wowote katika uasilishaji wa mashairi ya waandishi hawa. Utafiti huu ulichunguza mitindo katika diwani za Kichomi (1974) na Karibu ndani (1988) za Euphrase Kezilahabi na Msimu wa Tisa (2007) na Bara Jingine (2001) za Kithaka Wa Mberia. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Kimtindo inayosisitiza umuhimu wa lugha kama nyenzo kuu ya kupitisha ujumbe wa mtunzi kwa hadhira na wasomaji. Mtafiti aliongozwa na mihimili ya nadharia hii kutafuta data iliyotimiza malengo ya utafiti. Mtindo ni muhimu sana katika kazi yoyote ya fasihi kama vile mashairi. Waandishi wa mashairi huru wamekuwa wakitumia mitindo ya jazanda, taswira na takriri kwa kazi zao nyingi bila kutambua kuwa ni mitindo sawia wanayoitumia. Kipengele hiki kinahitaji kutafitiwa ili kuweka bayana kuwa katika mashairi huru waandishi huishia kutumia kaida fulani bila kujua. Utafiti ulifanywa maktabani na kwenye mtandao. Data iliteuliwa kwa njia ya kimaksudi kwa ambavyo inalenga washairi wawili, Kezilahabi na Kithaka Wa Mberia. Zaidi ya hayo tulitumia vitabu, makala mbalimbali na tasnifu za watafiti wengine. Inatarajiwa ya kwamba kazi hii itakuwa muhimu kwa watafiti, wasomi na watunzi wa mashairi. Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza ni utangulizi ambapo mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, suala la utafiti pamoja na upeo wa utafiti huu zimeshughulikiwa. Aidha, udurusu wa maandishi yanayohusu mada hii pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti huu imejadiliwa. Sura ya pili imeshughulikia mbinu za utunzi wa mashairi na fasihi kwa jumla. Hapa aina mbalimbali za mitindo ya uandishi zimetambuliwa na mifano kutolewa. Sura ya tatu imeshughulikia uainishaji wa mtindo wa taswira kwa kutumia mashairi huru. Imebainisha aina ya mitindo ya taswira iliyotumika katika mashairi ya Kezilahabi na Mberia. Sura ya nne imeshughulikia uainishaji wa mtindo wa jazanda kwa kutumia mashairi huru. Hali kadhalika, sura hii imebainisha aina ya mitindo ya jazanda iliyotumika katika mashairi haya. Sura ya tano imeshughulikia uainishaji wa mtindo wa takriri kwa matumizi ya mashairi huru. Vivyo hivyo, mifano ya takriri katika mashairi imetolewa. Sura ya sita ni hitimisho inayotoa muhtasari na matokeo ya utafiti huu, pamoja na mapendekezo ya utafiti. Mwisho kabisa, kuna marejeleo yaliyotumika katika utafiti huu.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 13 Mar 2018 13:00
Last Modified: 13 Mar 2018 13:00
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/3523

Actions (login required)

View Item View Item