Usambamba katika Ushairi-Huru

Mwania, James M. (2007) Usambamba katika Ushairi-Huru. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Usambamba katika Ushairi-Huru)
Mwania, James M..pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (75MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu umeshughulikia usambamba katika ushairi hum wa . Kiswahili. Lengo la utafiti huu ni kudhihirisha namna mshairi wa kisasa anavyotumia uhuru wake wa utunzi katika kujadili maswala mbalimbali yanayoikumba jamii. Utafiti huu umetumia usambamba katika kuzihakiki diwani za Kichomi, Mchezo wa Karata na Chembe cha Mayo. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia ya semiotiki. Nadharia hii huzingatia zaidi ishara na uashiriaji katika kazi za fasihi. Hivyo \ humsaidia mhakiki kuchunguza ujumbe unaowasilishwa na msann katika kazi zake. Kazi hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti pamoja na sababu za kuchagua mada. Hali kadhalika, udurusu wa maandishi yanayohusu mada ya utafiti pamoja na msingi wa nadharia iliyoongoza utafiti huu ni baadhi ya mambo ambayo yameshughulikiwa. Pia imeshughulikia mbinu za utafiti, sampuli, ukusanyaji pamoja na uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Sura ya pili imeshughulikia historia fupi ya ushairi pamoj a na dhana ya ushairi, ushairi hum na historia fupi ya ushairi hum. Kadhalika, mazingira ya msanii, enzi ya ukoloni katika Afrika Mashariki na kuchipuka kwa usambamba nchini Tanzania na Kenya ni baadhi ya yaliyojadiliwa. Pia imeshughulikia maisha ya wasanii tuliochunguza kazi zao Kezilahabi, Mberia na Mazrui. Sura ya tatu imeshughulikia usambamba na misimbo mbalimbali inayodhihirisha huo usambamba. Pia imeshughulikia uchimuzi na ukiushi. Sura ya nne imeshughulikia uradidi na utata pamoja na misimbo mbalimbali, inayotumika kuudhihirisha usambamba. Sura ya tano na ambayo ndiyo ya mwisho imeshughulikia muhtasari wa tasnifu, matokeo ya utafiti, pamoja na mapendekezo ya kufanyia utafiti zaidi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 15 Mar 2018 07:51
Last Modified: 15 Mar 2018 07:51
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/3529

Actions (login required)

View Item View Item