Kilauni, Nicholas W. (2007) Usasa katika Ngoma ya Itheke. Masters thesis, Kenyatta University.
PDF (Usasa katika Ngoma ya Itheke)
Kilauni, Nicholas W..pdf - Accepted Version Restricted to Repository staff only Download (71MB) | Request a copy |
Abstract
Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kutathmini usasa katika ngoma ya ltheke. Utafiti ulifanywa ili kubainisha jinsi usasa unavyoisaidia ngoma ya ltheke kuimarika na kuwa maarufu miongoni mwajimii ya Wakamba. Aidha utafiti ulidhamiria kubainisha jinsi usasa unavyoiwezesha ngoma ya Itheke kutekeleza majukumu ya kijamii. Nadharia za usasa na uamali zimetumiwa kwa pamoja katika utafiti huu. Nadharia ya usasa imetuongoza kubainisha jinsi usasa unavyodhihirika katika vipengele vya ngoma ya Itheke ambavyo ni: lugha na mtindo, ~udhyi, muktadha, teknoljia ya kisasa, hadhira, ala na maleba, Nadharia ya uamali hasa kipengele cha Ethnografia ya mazungurnzo kilitumika kubainisha jinsi vipengele vya ngoma ya Itheke vinavyotekeleza majukumu ya kijamii miongoni mwa jamii ya Wakamba. IIi kubainisha jinsi jamii ya Wakamba imekuwa ikikua na kubadilika, historia ya chimbuko la jamii Wakamba imedokezwa. Mabadiliko yalionekana kuadhiri mifumo yote ya kimaisha ikiwa ni pamoja na fasihi simulizi ya jamii ya Wakamba. Kwa sababu ya mabadiliko ya maisha, ngoma nyingi katika jamii ya Wakamba zimedidimia huku zingine zikiibuka. Ngoma ya ltheke m mojawapo ya ngoma zilizoibuka na kuwa maarufu kwa sababu ya usasa. Utafiti huu umeonyesha sababu za ngoma ya ltheke kuwa maarufu wakati ngoma zingine zinapodidimia na kusahaulika.
Item Type: | Thesis (Masters) |
---|---|
Subjects: | M Music and Books on Music > ML Literature of music P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania |
Divisions: | Africana |
Depositing User: | Tim Khabala |
Date Deposited: | 15 Mar 2018 07:46 |
Last Modified: | 15 Mar 2018 07:46 |
URI: | http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/3530 |
Actions (login required)
View Item |