M'Ngaruthi, Timothy Kinoti (2008) Usawiri wa Wahusika katika Dafina ya Umalenga (H.M. Mbega) na Jicho la Ndani (S.A. Mohamed). Masters thesis, Kenyatta University.
PDF (Usawiri wa Wahusika katika Dafina ya Umalenga (H.M. Mbega) na Jicho la Ndani (S.A. Mohamed))
M'Ngaruthi, Timothy Kinoti.pdf - Accepted Version Restricted to Repository staff only Download (75MB) | Request a copy |
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia swala la usawm wa wahusika katika mashairi ya Kiswahili. Mtafiti ameyahakiki mashairi teule ya washairi .wawili kwa lengo la kutathmini jinsi washairi hawa walivyowateua wahusika wao, aina za wahusika na jinsi wahusika hawa walivyotumiwa kutolea hisia za w,ashairi. Diwani zilizochaguliwa ni mbili; moja ya Hassan Mwalimu Mbega Dafina ya Umalenga (1984) na nyingine ya Said Ahmed Mohamed Jicho la Ndani (2002). Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile ya Ulimbwende ambayo hujaribu kueleza umuhimu wa wahusika katika ushairi, hasa katika kutolea hisia za mshairi badala ya kujifunga na arudhi. Nadharia hii pia hueleza umuhimu wa kuzin tia mazingira ya aina mbalimbali katika utunzi wa mashairi. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambapo mtafiti ameifafanua mada ya utafiti, sababu za kuchagua mada na upeo wa utafiti. Sura hii pia inao ufafanuzi juu ya udurusu wa maandishi yanayohusu mada hii pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti. Hatimaye pana maelezo juu ya mbinu za utafiti zilizotumika. Katika sura ya pili pamejadiliwa vigezo vinavyozingatiwa na washairi katika uteuzi wa wahusika wao. Mtafiti ameshughulikia aina mbalimbali za mazingira ambayo huchangia katika uteuzi wa wahusika. Sura ya tatu imejadili aina za wahusika wanaopatikana katika mashairi teule na jinsi washairi walivyowaunga kwa ubunifu wa hali ya juu kwa lengo la kuuwasilisha ujumbe wao kikamilifu. Mtafiti ameangaha jinsi wahusika hawa wanavyohusiana na kuathiriana na hivyo kusaidia katika ujenzi wa maudhui. Katika sura ya nne mtafiti amejadili jinsi washairi walivyowatumia wahusika kudhihirishahisia mbalimbali. Sura ya tano ni hitimisho linalotoa muhtasari na matokeo ya utafiti, pamoja na mapendekezoya mtafiti. Mwishonimwa tasnifu kuna marejeleo ya utafiti huu.
Item Type: | Thesis (Masters) |
---|---|
Subjects: | P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania |
Divisions: | Africana |
Depositing User: | Tim Khabala |
Date Deposited: | 15 Mar 2018 07:45 |
Last Modified: | 15 Mar 2018 07:45 |
URI: | http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/3531 |
Actions (login required)
View Item |