Usawiri wa Wahusika Makahaba katika Riwaya za Said Ahmed Mohammed

Muindi, Augustine (1990) Usawiri wa Wahusika Makahaba katika Riwaya za Said Ahmed Mohammed. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Usawiri wa Wahusika Makahaba katika Riwaya za Said Ahmed Mohammed)
Muindi, Augustine.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (59MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti wetu unahusu suala la ukahaba katika rlwaya nne za Said Ahmed Mohamed. Tunahakiki usawiri wa wahusika makahaba kwa madhumuni ya kubainisha sababu za kuwepo kwa ukahaba katika jamii. Aidha, tunatilii namna ambavyo mwandishi anawabadilisha wahusika wake kutoka kwa maisha ya ukahaba na kama mabadiliko hayo yanatoasuluhisho halisi kwa jamii ya makahaba. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo tunapojadili tasnifu kwa jumla, mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti wetu, upeo wa utafiti wetu. Vile vile, tunajadili baadhi ya kazi nyingine zilizowahi kuandikwa na ambazo kwa namna fulani, zinahusiana na utafiti wetu. Aidha, tutasema machache kuhusu nadharia tunayotumia katika utafiti wetu. Kisha tutatazama sababu za kuchagua mada hii na njia tutakazofuata katika kutafiti juu ya mada yetu. Katika sura ya pili na ambayo ndiyo nguzo ya utafiti, tunaelezea dhana na nadharia za ukahaba. Dhana na nadharia hizi zinatusaidia katika kubainisha vigezo mbalimbali vinavyotambulisha kahaba katika jamii. Tunafikia upeo wa utafiti wetu katika sura ya tatu na nne. Katika sura ya tatu, tunanuia kubainisha sababu mbalimbali ambazo zimewavuta baadhi ya wahusika katika maisha ya ukahaba. Sura ya nne, tunajadili namna ambavyo mwandishi anawaondoa wahusika wake kutoka kwa maisha hayo. Sura ya tano ni ya hitimisho. Tunatoa muhtasari wa kazi tuliyoifanya. Kisha, tunatathmini kama tumefikia malengo ya utafiti wetu. Mwisho-kabisa, tunatoa marejeleo ya utafiti wetu.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: H Social Sciences > HQ The family. Marriage. Woman
H Social Sciences > HV Social pathology. Social and public welfare
P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 15 Mar 2018 07:42
Last Modified: 15 Mar 2018 07:42
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/3540

Actions (login required)

View Item View Item