Uhakiki wa Kimtindo wa Nyimbo za Mazishi Miongoni Mwa Wakamba

Esther, Eunice Musyoka (2012) Uhakiki wa Kimtindo wa Nyimbo za Mazishi Miongoni Mwa Wakamba. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Uhakiki wa Kimtindo wa Nyimbo za Mazishi Miongoni Mwa Wakamba)
2016-02-120.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (85MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu ulidhamiria kufafanua tamathali za lugha zinazotumiwa katika nyimbo zinazoimbwa katika muktadha wa mazishi ya Kikristo ya jamii ya Wakamba, wakati wa kuwasilisha ujumbe kupitia nyimbo. Lugha iliyotumiwa katika nyimbo hizo huwa teule na yenye ukwasi mkubwa wa tamathali za usemi kama vile: jazanda, taswira, tashihisi, tashbihi, takriri na maswali ya balagha miongoni mwa zingine. Kimsingi matumizi hayo huvuta hisi za hadhira kwa njia ya pekee. Aidha, utafiti huu ulilenga kubainisha ujumbe unavyowasilishwa kupitia tamathali za lugha, ili kuibua mielekeo yajamii ya Wakamba kuhusu kifo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mtindo na ya Ethnografia ya Mawasiliano. Mihimili mitatu ya nadharia ya Mtindo namhimili mwingine mmoja wa Ethnografia ya Mawasiliano iliunganishwa ili kuunda mihimili minne mahususi iliyotumiwa katika uchanganuzi wa data. Utafiti huu ulifanywa ili kubainisha dhima ya matumizi ya tamathali za lugha katika uwasiiishaji wa ujumbe katika nyimbo za mazishi ya Kikristo ya Wakamba. Aidha utamaduni wa jamii hii haujadidimia kabisa kwa sababu, athari yake bado ina nguvu katika jamii. Maoni hayo yamedhihirishwa kupitia kwa mielekeo inayoibuliwa n(l kauli teule katika nyimbo hizo. Kwa ambavyo utanzu wa nyimbo za mazishi haujafanyiwa utafiti wa kina katika jamii ya Wakamba, utafiti huu umetoa mchango kuhusu utanzu huo wa fasihi simulizi. Kwa vile umefanunua baadhi ya tamathali muhimu za lugha zilizoshirikishwa katika uwasiiishaji wa utanzu huu katika eneo la Thaana Nzau. Data i1ikusanywa nyanjani katika wilaya ya Migwani, tarafa ya Thaana Nzau. Udurusu wa vitabu na majarida maktabani ulisaidia katika kupata maelezo ya baadhi ya tamathali zalugha, najinsi ya kuzitumia katika muktadha wake. Mbinu ya ukusanyaji wa data ilizingatia uchanganuzishirikishi pamoja na mahojiano. Data ilichanganuliwa kwa kuzingatia tamathali maalum za lugha, ujumbe, malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia zilizozingatiwa Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: B Philosophy. Psychology. Religion > BL Religion
G Geography. Anthropology. Recreation > GV Recreation Leisure
M Music and Books on Music > M Music
Divisions: Africana
Depositing User: Geoffrey Obatsa
Date Deposited: 03 Feb 2017 10:45
Last Modified: 03 Feb 2017 10:45
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/1416

Actions (login required)

View Item View Item