Viwango vya Uhalisi na Ubunifu Katika Riwaya Teule za Kiswahili

Lomatoro, P. Joel (2014) Viwango vya Uhalisi na Ubunifu Katika Riwaya Teule za Kiswahili. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Viwango vya Uhalisi na Ubunifu Katika Riwaya Teule za Kiswahili)
2016-02-146.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (79MB) | Request a copy

Abstract

Katika utafiti huu, tumeshughulikia viwango vya uhalisi na ubunifu katika riwaya teule za Kiswahili: Cheche za Moto (2008) ya Habwe John, Kaburi BUa Msalaba (1969) ya Kareithi P.M. na Kusadikika (1951) ya Shaaban Robert.IIi kuafiki hili, tumeangalia mbinu zilizotumiwa na waandishi kusawiri uhalisia na ubunifu katika riwaya za Kiswahili. Kila mwandishi ana njia yake ya kipekee ya kuwasilisha kazi yake. Kuna wanaoeleza yaliyotendeka katika jamii kwa uaminifu na kwa narnna ambayo atakayesoma kazi yake ataona ni mambo yanayosadikika au yaweza kutendeka katika jamii. Njia zinazotumiwa na waandishi kama hao zimeangaziwa katika utafiti huu. Zaidi ya hayo kuna waandishi wanaovuta fikra zao na kusimulia visa ambavyo vinaonekana kuwa ni vya kufikirika tu wala haviwezi kutendeka katika ulimwengu halisi. Kazi hizo ndizo tumeita 'ubunifu' katika utafiti huu. Hivyo basi kazi hii imejaribu kuangazia mbinu hizo na kuona iwapo kuna uhusiano wowote kati ya kazi hizo za kihalisia na kibunifu. Katika kuangalia uhusiano huo, utafiti huu umeangalia namna ambavyo waandishi wa rriwaya zilizotajwa, wameeleza visa 'kibunifu' na namna ambavyo uhalisia unajitokeza katika 'ubunifu' huo. 'Ubunifu' unaojitokeza katika kazi za kihalisi pia umeangaziwa. Nadharia iliyotumiwa ni nadharia ya uhalisia. Nadharia hii imechaguliwa kwa misingi kuwa mihimili yake itatuwezesha kuchambua vitabu vilivyoteuliwa na kuafiki malengo ya utafiti. Data ya utafiti ilipatikana kwa kusoma vitabu vyote vilivyochaguliwa na yaliyoangaliwa ni namna waandishi wamewasawiri wahusika wao, matukio na mandhari yao. Uchanganuzi ulifanywa kwa njia ya maelezo na mahitimisho kutolewa kimaelezo. Utafiti huu umeeleza nafasi ya uhalisi na ubunifu katika maendeleo ya riwaya za Kiswahili. Utatoa mchango katika uchambuzi wa riwaya za Kiswahili na matokeo yake kutumiwa katika kuainisha riwaya hizo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > PI Oriental languages and literatures
P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
P Language and Literature > PN Literature (General)
Divisions: Africana
Depositing User: Geoffrey Obatsa
Date Deposited: 28 Apr 2017 12:20
Last Modified: 28 Apr 2017 12:20
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/1451

Actions (login required)

View Item View Item