Matumizi ya Lugha katika Nyimbo Tohozi za Salim Junior

Mwaniki, Margaret W (2011) Matumizi ya Lugha katika Nyimbo Tohozi za Salim Junior. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Matumizi ya Lugha katika Nyimbo Tohozi za Salim Junior)
Matumizi ya lugha katika nyimbo tohozi za Salim Junior.pdf
Restricted to Repository staff only

Download (56MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu umeshughulikia uchanganuzi wa nyimbo ambazo Salim Junior ametohoa. Katika sura ya kwanza, tumetoa utangulizi wa utafiti wetu. Tumetoa usuli wa utafiti, swala la utafiti, malengo ya utafiti, upeo wa utafiti, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada miongoni mwa mengine. Kwa jumla, swala la utafiti limejadiliwa. Kutokana na utangulizi, imebainika kwamba pengo lilikuwepo, nalo lilikuwa kuonyesha jinsi Salim Junior anavyotohoa nyimbo za wasanii wengine. Katika sura ya pili, tumefafanua sababu za kuangazia wasifu wa Salim Junior na umuhimu wa wasifu huu kwa utafiti wetu. Tumetoa wasifu wa mwimbaji Salim Junior na mazingira alimokulia. Tumejadili namna alivyoingia katika uwanja wa muziki na maendeleo aliyoyapara na pale ambapo amefikia kwa sasa. Sehemu hii imeonyesha maisha ya msanii . ni muhimu katika ufahamu wa sanaa yake. Katika sura ya tatu, tumetanguliza kwa kueleza umuhimu wa kujadili historia na mabadiliko ya kipera cha nyimbo katika jamii ya Wakikuyu ambao ndio msingi wa nyimbo za Salim Junior. Tumeendelea kwa kujadili mabadiliko ambayo yamepatikana katika kipera cha nyimbo katika jamii ya Wakikuyu tangu na kabla ya wageni kufika katika sehemu za Ukikuyuni hadi sasa. Tumepitia vipindi vinne vya kihistoria na kuangazia mabadiliko kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Sura hii imeonyesha kwamba utohozi ni sehemu ya usanii katika nyimbo za Kikuyu. Katika sura ya nne, tumechanganua nyimbo ambazo mwimbaji huyu ametohoa kutoka kwa lugha yake ya Kikuyu. Tumejadili pia wimbo ambao mwimbaji ametohoa midundo yake kutoka kwa lugha ya Kiluhya na tumemalizia kwa wimbo wa watoto. Tumemalizia kwa sura ya tano ambapo tumetoa muhtasari wa kazi hii, matokeo ya utafiti huu na mapendekezo yetu. Tumeyapitia matatizo tuliyokumbana nayo katika utafiti huu na namna tulivyokabiliana nayo. Mwisho, tumehitimisha kwa kutoa inapendekezo ya tafiti zingine zinazoweza kufanywa katika uwanja huu. Kutokana na utafiti huu, imedhihirika kwamba utohozi ni kiungo cha kawaida katika usanii wa nyimbo za Kikuyu. Pili, imebainika kwamba si Salim Junior pekee ambaye anatohoa nyimbo za wasanii wengine, lakini kuna wasanii wengine wanaofanya vivyo hivyo. Vile vile, imebainika kuwa dhana ya kanivali inaweza kutumiwa kufafanua vizuri zaidi namna nyimbo za wasanii wa Kikuyu zinavyotoholewa. Uwezo wa kanivali kuhakiki nyimbo hizi unatokana na usemezano na mwingiliano matini uliomo katika nyimbo hizo. Tunaweza pia kusema kuwa nyimbo ni mali ya jamii na ndiyo sababu msanii anaweza kutohoa kwa urahisi zaidi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: M Music and Books on Music > ML Literature of music
P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 20 Nov 2017 10:20
Last Modified: 20 Nov 2017 10:20
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/2713

Actions (login required)

View Item View Item