Maigizo katika Fasihi Simulizi: Mfano wa Kirarire katika Nyimbo za Tohara za Wameru

Mutegi, Lewis (2010) Maigizo katika Fasihi Simulizi: Mfano wa Kirarire katika Nyimbo za Tohara za Wameru. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Maigizo katika Fasihi Simulizi: Mfano wa Kirarire katika Nyimbo za Tohara za Wameru)
Mutegi, Lewis.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (51MB) | Request a copy

Abstract

Mada ya utafiti huu m maigizo katika fasihi simulizi kwa kurej elea mifano kutoka kirarire katika nyimbo za tohara za Wameru. Mtafiti ameangazia umuhimu wa maigizo katika utanzu huu wa nyimbo kwa lengo la kudhihirisha jinsi ambavyo wahusika katika nyimbo hizi huwasilisha ujumbe wao kwa njia ya ubunifu. Mtafiti pia alinuia kuwaonyesha baadhi ya watafiti wa awali ambao hushikilia kuwa hakuna maigizo katika bara la Afrika kwamba kweli yapo. Utafiti huu uliongozwa na Nadhariaya Maigizo ambayo husisitiza umuhimu wa kuonyesha mitagusano ya wanajamii katika maisha yao halisi kupitia vitendo vya jukwaani. Nadharia hii pia huonyesha umuhimu wa hadhira katika kuwatathmini waigizaji wanapoendelea na vitendo vyao jukwaani. Tasnifu hii imegawanywa katika _sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa tasnifu. Hapa, mtafiti ameifafanua mada ya utafiti, sababu za kuchagua mada na upeo wa utafiti. Udurusu wa maandishi pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti pia zimefafanuliwa. Mbinu za utafiti zilizotumiwa katika utafiti huu zimefafanuli wa. Sura ya pili inaangazia historia ya jamii ya Wameru ambao ndio watafitiwa. Mtafiti amefafanuamifumo ya kisiasa na kijamii ya Wameru, fasihi simulizi na utamaduni wao pamoja na vipawa vyao vya kisanii. Lengo kuu hapa ni kudhihirisha kuwa ingawa bara la Afrika limepitia mabadiliko makubwa ya kitamaduni, bado kuna jamii ambazo zingali zinauthamini utamaduni wake. Sura ya tatu i?1echunguza sifa za maigizo katika kirarire. Baadhi ya yaliyoshughulikiwa ni njia ya mawasiliano, jukwaa, tukio la kuigizwa, mila na tamaduni zinazohusika na ujumi na itiksadi ya mawasiliano katika kirarire. Sura ya mwisho inatoa muhtasari wa matokeo, hitimisho na mapendekezo ya utafiti. Hatimaye kuna marejeleo ya utafiti huu.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: M Music and Books on Music > ML Literature of music
P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 15 Dec 2017 13:51
Last Modified: 15 Dec 2017 13:51
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/2955

Actions (login required)

View Item View Item