Uchunguzi wa Uozo katika Mashairi ya Khatib na King'ei

Barasa, Ayub Oyimba (2015) Uchunguzi wa Uozo katika Mashairi ya Khatib na King'ei. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Uchunguzi wa Uozo katika Mashairi ya Khatib na King'ei)
Barasa, Ayub Oyimba.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (55MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu umeshughulikia uozo katika mashairi ya Khatib na King'ei kwa kuongozwa na nadharia ya kimtindo na maadili. Nadharia hizi zilifaa utafiti huu ikizingatiwa kwamba maudhui ya mtunzi na mtindo anaoutumia katika kutoa ujumbe wake ni vipengele vinavyotegemeana. Mtunzi hutunga kutokana na tajriba aliyopata katika mazingira yake na lugha ndiyo aitumiayo kueleza mambo mbalimbali ya jamii yake kwa njia ya kubuni. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza imetupa mwelekeo wa utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchagua mada. Hali kadhalika sura hii imeshughulikia misingi ya nadharia, upeo na mipaka na yaliyoandikwa kuhusu mada. Mwisho ni mbinu za utafiti na uchanganuzi wa data. Sura ya pili imejadili mashairi yenye uozo wa kijamii kama vile ndoa, mapenzi, dini, utamaduni na falsafa kuhusu maisha. Tumeonyesha narnna maudhui ya uozo kijamii yalivyojengwa kifani na mafunzo waliyotoa watunzi. Sura ya tatu imejadili uchambuzi wa mashairi yenye maudhui ya uozo wa kisiasa. Tumeonyesha jinsi maudhui haya ya watunzi hawa yalivyosababisha uteuzi maalum wa lugha katika kuyaibusha. Sura ya nne imejihusisha na uchambuzi wa mashairi yenye maudhui ya uozo wa kiuchumi. Katika sehemu hii, tumeonyesha jinsi mtindo maalum wa mwandishi unavyosadia kuibusha ujumbe wake na mafunzo wanayotoa waandishi kurekebisha hali ya uozo. Sura ya tano ni hitimisho. Sura hii ni muhtasari wa matokeo ya utafiti wetu ambamo licha ya kueleza ugunduzi wa uchambuzi wetu tumetoa kauli yetu juu ya umuhimu wa utafiti wetu na maeneo ambayo yanastahili kufanyiwa utafiti zaidi hapo baadaye.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 13 Mar 2018 13:09
Last Modified: 13 Mar 2018 13:09
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/3519

Actions (login required)

View Item View Item