Uhakiki wa Tamthilla ya Watoto kama Zao la Michezo ya Utotoni

Ojiambo, Bwire Thedius (2004) Uhakiki wa Tamthilla ya Watoto kama Zao la Michezo ya Utotoni. Masters thesis, University of Nairobi.

[img] PDF (Uhakiki wa Tamthilla ya Watoto kama Zao la Michezo ya Utotoni)
Bwire_Uhakiki wa tamthilia ya watoto kama zao la michezo ya utotoni.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (5MB) | Request a copy

Abstract

Kazi hii inashughulikia tamthilia ya watoto kama zao la michezo au maigizo ya utotoni. Kuna sura tano katika tasnifu hii. Kuna tanbihi mwishoni mwa sura ya kwanza, ya pili, ya tatu na ya nne. Baada ya sura ya tano, kuna orodha ya vitabu vya marejeleo na mwishoni kabisa, viambatisho.Sura ya kwanza inatanguliza kazi nzima. Katika sura hii, tumeonyesha tatizo la utafiti, kusudi la utafiti, sababu za kuchagua mada hii, mipaka ya utafiti na msingi wa nadharia. Utafiti huu umeongozwa na kanuni za nadharia ya semiotiki ambayo inajishughulisha na ishara na maana ya ishara hizo katika kazi ya kifasihi. Aidha kumeonyeshwa mbinu za utafiti tulizozitumia.Sura ya pili inashughulikia hali ya michezo au maigizo ya utotoni nchini. Hapa, tumeonyesha ushiriki wa watoto katika michezo ya utotoni, viambajengo vya michezo hiyo na hatimaye tumetoa ufafanuzi kuhusu dhima ya michezo hii maishani mwa watoto.Sura ya tatu imesheheni uhakiki wa maudhui muhimu katika tamthilia nne teule zilizowasilishwa na watoto wa shule za msingi katika tamasha za drama za mwaka 2002. Tamthilia hizo ni Tuzo Azizi, Majuto, Monalisa na Vososauti. Tumeonyesha kuwa maudhui yanayoshughulikiwa na tamthilia hizo yana mshabaha na maudhui yanayoshughulikiwa katika michezo ya utotoni. Pia tumemulika ukweli kwamba fasiri ya baadhi ya watunzi ya maudhui hayo haijalingana na urazini wa watoto-lengwa bali i katika mawanda ya watu wazima.Katika sura ya nne, tumejishughulisha na uchanganuzi wa wahusika pamoja na matumizi yao ya lugha katika tamthilia hizo teule. Tumebainisha kuwa vipengele hivi vya fani; yaani usawiri wa wahusika na matumizi yao ya lugha, vyote havilingani na urazini wa watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na mitatu.Sura ya tano ni hitimisho. Katika sura hii, tumetoa maoni yetu kuhusu maswala tuliyoyashughulikia katika tasnifu hii pamoja na kupendekeza njia za kuiboresha drama ya watoto. Aidha, tumetoa mapendekezo ya kufanywa kwa utafiti zaidi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Depositing User: Geoffrey Obatsa
Date Deposited: 21 Jul 2016 08:21
Last Modified: 21 Jul 2016 08:21
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/755

Actions (login required)

View Item View Item