Ufaafu wa Maana katika Tafsiri ya Nyimbo Dini

Ondara, Kiyondi Reuben (2010) Ufaafu wa Maana katika Tafsiri ya Nyimbo Dini. Masters thesis, Kenyatta University.

[img] PDF (Ufaafu wa Maana katika Tafsiri ya Nyimbo Dini)
Ondara, Kiyondi Reuben.pdf - Accepted Version
Restricted to Repository staff only

Download (72MB) | Request a copy

Abstract

Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza ufaafu wa maana katika tafsiri za nyimbo dini za Kiswahili. Nyimbo kumi za watunzi watatu ziliteuliwa kama matini chasili, na tafsiri yao katika vitabu viwili, Nyimbo Standard (1897,2005) na Nyimbo Za Kristo (Mwaka Haujatolewa), ikachukuliwa kama matini lengwa. Nadharia ya Uhusiano iliyoasisiwa na Sperber na Wilson (1986) pamoja na mihimili yake ilitumiwa kama dira ya kuelekeza kazi hii. Utafiti ulifanywa maktabani ambapo vitabu, majarida na tasnifu mbalimbali zilipitiwa, na data iliyopatikana ikachanganuliwa na kuwasilishwa kwa maelezo ya kinathari. Kutokana na utafiti huu, imebainika kuwa mtafsiri wa nyimbo dini hizi kwa Kiswahili, amejaribu sana kutafsiri kikamilifu maana ya nyimbo asilia, lakini maana katika baadhi ya nyimbo zilizotafsiriwa ina upungufu na hivyo kwa kiwango kikubwa, haifai. Hii ni kutokana na kutozingatia suala la sarufi, tafsiri isiyoridhisha ya tamathali za usemi pamoja na kuongeza, kuondoa na kubadilisha maana asilia katika nyimbo lengwa. Tasnifu hii ina sura tano ambazo zimegawa .kwa njia ifuatayo: Sura ya kwanza inajumuisha vipengele muhimu vya utafiti kama vile, utangulizi, suala na malengo ya utafiti, tahadhania, msingi wa nadharia, mbinu za utafiti pamoja na mapitio ya maandishi mbalimbali. Sura ya pili inatoa historia ya nyimbo dini na ya watunzi walioteuliwa na maelezo machache kuhusu nyimbo zilizoteuliwa. Sura ya tatu na ya nne zinatoa tahakiki ya nyimbo zilizoteuliwa kwa kuzingatia vipengele kama vile maana, msamiati, sarufi na tamathali za userni, na vile zimetumika katika tafsiri ya nyimbo dini. Sura ya tano inatoa hitimisho la utafiti kwa kutoa matokeo ya utafiti na mapendekezo, na mwisho wa tasnifu, marejeleo pamoja na viambatisho mbalimbali vimetolewa.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: B Philosophy. Psychology. Religion > BR Christianity
M Music and Books on Music > ML Literature of music
P Language and Literature > PL Languages and literatures of Eastern Asia, Africa, Oceania
Divisions: Africana
Afro-Christiana
Depositing User: Tim Khabala
Date Deposited: 13 Mar 2018 13:06
Last Modified: 13 Mar 2018 13:06
URI: http://thesisbank.jhia.ac.ke/id/eprint/3520

Actions (login required)

View Item View Item